Friday, June 26, 2015

Houston kufanya Harambee ya Kusafirisha mwili wa Mar.Edmund Mushi Jumamosi 27th June

Marehemu Edmund Mushi

Wanajumuiya,

Kamati iliyopewa jukumu la kutafuta ukumbi wa Harambee imefanikisha suala hilo. Harambee kwa ajili ya kuchangisha pesa zitakazowezesha kusafirisha mwili wa ndugu yetu, marehemu Edmund Mushi, itafanyika siku ya Jumamosi June 27, 2015 kama ilivyopangwa.

Address ya ukumbi ni 9423 Highway 6 Houston, TX 77083. Muda ni saa 10 alasiri mpaka saa 2 jioni.

Bajeti nzima ya kuwezesha kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi ni USD$21,100.00. Tunaomba kila mmoja wetu kuhakikisha tunawezesha kufanikisha kwa gharama hizi.

Tunaombwa tuje na vyakula kwa akina mama na vinywaji kwa akina baba. Tunahimiza pia kuanza kutoa michango yetu mapema ili kurahisisha zoezi hili.

Wells Fargo Bank
Edmund Lawrence Memorial Fund
Account 6519426271
Routing 111900659
For non Wells Fargo account holders use routing 121000248


Asanteni.

Arnold Maira,
THC-Interim Spokesman.


Tuesday, June 23, 2015

Msiba Houston, Texas

Marehemu Edmund Mushi enzi za uhai wake
Wanajumuiya,

Kwa masikitiko makubwa, tunasikitika kutangaza kifo cha mwanajumuiya mwenzetu 
Bw. Edmund Mushi.

Ndugu yetu Edmund amefikwa na mauti usiku wa kuamkia leo June 23, 2015 katika hospital ya Houston Northwest Medical Center alipokuwa amelazwa.

Tunatoa wito kwa wanajumuiya kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Taarifa zaidi za hatua itakayofuata zitatolewa mara tu baada ya kumalizika kwa kikao cha wanandugu wa karibu baadaye mchana huu.

Kwa niaba ya Jumuiya, tunatoa pole kwa ndugu, jamaa, na marafiki wa marehemu.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi

Asanteni,

Arnold Maira,
THC-Interim Spokesman.