Monday, August 22, 2016

TIGO FIESTA 2016 YAZIZIMA JIJINI MWANZA

Mkali wa singeli ManFongo na Shilole wakilivamia jukwaa la Tigo Fiesta 2016 katika tamasha hilo kubwa liliofanyika usiku wa  jana jijini Mwanza na kukutanisha wasanii nguli katika muziki wa kizazi kipya na Msanii wa kimataifa  toka Nigeria Wizkid
Umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza wakitoa shangwe wakati burudani mbalimbali zikiendelea katika Tamasha la Tigo Fiesta 2016  viwanja vya CCM Kirumba hapo usiku wa jana
Alikiba alikuwa kivutio kwa mashabiki wengi mara baada ya kufanya suprize na kutoa burudani ya kukata na shoka huku mashabiki zake wakifuatisha nyimbo zake moja baada ya nyingine katika Tamasha la Tigo Fiesta 2016 katika viwanja vya Kirumba Jijini Mwanza
Benpol akilishambulia jukwaa la Tigo Fiesta 2016 lilifnayika jana katika viwanja vya CCM kirumba Jijini Mwanza.
Msanii wa kizazi kipya Dayna Nyange akitumbuiza umati uliohudhuria Tamasha la Tigo Fiesta 2016 jijini Mwanza hapo usiku wa jana
Mkali wa Singeli anayetamba na nyimbo yake "HAINAGA USHEMEJi"  akitumbuiza jukwaa la Tigo Fiesta 2016 Jijini Mwanza.
Aika na Nahreel (Navykenzo ) nao walifanikiwa kuteka jukwaa la Tigo Fiesta 2016 Jijini Mwanza
Wasanii toka kikundi cha TipTop connections Tundaman na Madee Ali wakitumbuiza mashabiki katika jukwaa la Tigo Fiesta 2016  katika viwanja vya CCM kirumba hapo usiku wa jana .
Weusi wakilishambulia vilivyo  jukwaaa la Tigo Fiesta 2016 Jijini Mwanza hapo usiku wa jana
Msanii wa  kimataifa toka Nigeria Ayodeji Balogun(Wizkid) akitumbuiza katika tamasha la Tigo Fiesta 2016 liliofanyika hapo jana Jijini Mwanza  katika viwanja vya CCM Kirumba
Baadhi ya waandishi wa Habari wakichukua matukio katika tamasha la Tigo Fiesta 2016 wakazi msanii wa kimataifa toka Naijeria Wizkid akitumbuiza katika viwanja vya CCM kirumba usiku wa jana .


Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wakishangilia wakati burudani mbalimbali zikitolewa na wasanii waliotikisa jukwaaa la Tigo Fiesta 2016 hapo usiku wa jana katika viwanja vya CCM Kirumba Jijini Mwanza 


No comments:

Post a Comment