Monday, October 23, 2017

ZIARA YA MH. BALOZI MASILINGI JIJINI HOUSTON KATIKA PICHA

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mh. Balozi Wilson Masilingi siku ya jana Jumapili ya tarehe 22/10 alifanya ziara ya kikazi katika jiji la Houston katika jimbo la Texas na kukutana na Watanzania wanaoishi jijini humo .

Katika ziara hiyo pia Mh. Balozi Masilingi alikutana na familia zilizoathirika na kimbunga cha Harvey ambacho kililikumba jiji Jimbo la Texas mwezi Agosti mwaka huu. Mh. Balozi Masilingi vilevile alikabidhi mchango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa familia hizo ambazo zilipoteza mali na wengine makazi wakati wa kimbunga.

Mkutano na Wanajumuiya wote ulifanyika katika Ukumbi wa Hotel Marriott uliopo Briarpark Dr. Houston, Texas . Pata picha za mkutano huo hapa chini.

Mh. Balozi WIlson Masilingi akiongea na wana-Houston
Mh. Balozi Masilingi akiwasalimia Watanzania wa Houston

Rai wa Jumuiya ya Watanzania wa Houston (THC) akimkaribisha Mh. Balozi Masilingi

Mh. Balozi Masilingi akiwa na Rais wa THC Bw. Mayocha



Viongozi wa THC wakiwa na Mh. Balozi Masilingi, kutoka kushoto ni
Bw. Lambert Tibaigana (THC Vice President), Mh. Balozi,
Bw. Mayocha (THC President) na Bw. Cassius Pambamaji ( THC Spokesperson)




















Bw. Kasapira akiendesha mitambo




Afisa Ubalozi Bw. Bw. Alfred Swere akijitambulisha kwa wana-Houston




Meza kuu

































































No comments:

Post a Comment